1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Tshisekedi aanza kukabiliwa na changamoto

Saleh Mwanamilongo7 Februari 2019

Watumishi wa umma wataka nyongeza ya mishahara katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku shirika la kitaifa la utangazaji likitishia pia kujiunga na mgomo huo.

Kongo Felix Tshisekedi
Picha: picture-alliance/dpa/B. Curtis

Rais mpya nchini Congo, Felix Tshisekedi ameanza kukabiliwa na changa moto, ikiwa ni pamoja na madai ya watumishi wa umma kuongezewa mishahara. Watumishi hao wa umma wameanzisha mgomo huku shirika la kitaifa la utangazaji likitishia pia kujiunga na mgomo huo. Wafanya kazi hao wanadai kuondolewa kwa mkurugenzi wa shirika lao.

Maandamano na migomo kwa ajili ya kudai hali bora ya maisha vilianzishwa siku tatu tuu baada ya rais mpya kuapishwa. Mjini Lubumbashi, mji wa pili kwa ukubwa nchini Congo, wanafunzi wa chuo kikuu waliandamana kudai huduma bora ya maji na umeme kwenye chuo hicho. Polisi waliwatawanya kwa kutumia risasi ambako watu watatu wakiwemo wanafunzi wawili walifariki.

Mjini Kinshasa, wafanyakazi wa shirika la umma la usafiri wa basi, TRANSCO, waliagoma na kuandama kuomba mkurugenzi wa shirika hilo kujiuzulu kwa kile wanachotaja kuwa ni uongozi mbaya. Bila kusita, rais Felix Tshisekedi aliamuru kuachishwa kazi kwa Michel Kirumba, mkurugenzi wa Transco. Hali hiyo ikawapa motisha wafanya kazi wa mashirika mengine ya umma. Kwenye shirika mwenza la Usafiri wa reli, wafanya kazi wameomba pia kujiuzulu kwa mkurugenzi wa shirika hilo la SCTP, ONATRA.

Augustin Kalume anayefanya kazi kwenye shirika la TRANSCO amelezea kuwa mkurugenzi wa kampuni lao, alishindwa kuawajibika katika majukumu yake.

Shirika la kitaifa la utangazaji limetishia pia kushiriki mgomoPicha: DW/Wendy Bashi

"Ni toka mwaka 2015 ambapo tulianzisha mfululizo wa migomo ilikudai kuboreshewa hali yetu ya maisha. Lakini serikali iliondoka hailikujali malalamiko yetu. Mwenyewe mkurugenzi wetu alisema kwamba madai yetu yanamsingi wa kisiasa, huo ni uongo mtupu ». Amesema Augustine.

Mshangao umetokea kwenye redio na televisheni ya kitaifa ambako wafanya kazi wake wanatishia mgomo. Itakuwa ni mara ya kwanza waandishi habari kugoma kwenye televisheni ya taifa. Chama cha wafanya kazi wa kituo la utangazaji cha kitaifa,RTNC, kinaelezea kwamba ikiwa madai ya wafanya kazi hayatotekelezwa mgomo utaanzishwa wiki ijayo. Kwa nini mgomo huo umekuja kipindi hiki cha mageuzi ya uongozi ? Rene Kalonda kiongozi wa chama cha wafanya kazi wa RTNC amesema kwamba hatua hiyo inalenga kumuwekea shinikizo rais mpya.

Rene ameendelea kusema: "Mgomo huo ni madai ya wananchi, ni sawa na volcano ambayo ilizuiliwa kuripuka lakini mwishoe imetapika majivu ya moto. Kwa muda mrefu tuliomba kuwepo na mazungumzo baina ya mkurugenzi wa RTNC na na chama cha wafanya kazi.Lakini hakujali. Na leo kuwepo na rais mpya kunatupa motisha ya kudai nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kufanyia kazi ».

Hata hivyo wengi wanaamini kwamba ni mapema mno kusubiri majibu kuhusu nyongeza ya mishahara kwa rais mpya.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW