1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Rais Tshisekedi anaongoza katika matokeo ya awali

Hawa Bihoga
28 Desemba 2023

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku rais Felix Tshisekedi akiongoza kwa asilimia kubwa.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | Uchaguzi wa urais Kongo
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: AFP

Hadi usiku wa kuamkia leo, tume ya uchaguzi CENI ilitangaza matokeo ya kura zaidi ya milioni 9 ambazo tayari zimehisabiwa.

Katika matokeo hayo Rais Felix Tshisekedi anayewania muhula wa pili ameonekana kupata kura zaidi ya milioni saba ambazo ni sawa na asilimia 77 huku mpinzani wake wa karibu Moise Katumbi akiwa na asilimia 15 na Martin Fayulu akishika nafasi ya tatu sawa na asilimia 4 pekee.

Tshisekedi anaongoza kwa wingi wa kura katika majimbo 21 kati ya 26 ya Kongo pamoja na jiji kuu la Kinshasa naye Katumbi akiongoza katika majimbo manne ya kusini mashariki yakiwemo Haut-Katanga na Tanganyika.

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Rais yanatarajiwa kutangazwa jumapili ya Desemba 31.

Upinzani umeyapinga matokeo hayo ya awali na kusema yalipangwa na Tume ya uchaguzi ilikumpa ushindi Rais Tshisekedi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW