Putin "Ukraine lazima ikubaline na masharti yetu"
5 Julai 2024Putin amesema Ukraine inaweza kutumia nafasi ya usitishaji vita kujihami kwa mashambulizi mapya na hiyo ndiyo sababu kunabidi kwanza kufanyike mazungumzo ya kupata suluhisho endelevu.
Kiongozi huyo wa Urusi aliyasema hayo jana Alhamisi huku pia akigusia makubaliano yaliyofikiwa huko nyuma kuhusu vita hivyo vya Ukraine ambayo yaliishia kutupiliwa mbali.
Mtazamo wa Putin umekuja katika wakati ambapo viongozi wa Umoja wa Ulaya jana walizungumzia wasiwasi wao kuhusu tetesi kwamba waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban anayeshikilia uongozi wa Umoja huo kwa sasa, anajiandaa kwenda Moscow.
Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel amesema Orban hana mamlaka ya kuchukua hatua hiyo.Michel amesema Urusi ni mchokozi na Ukraine ni muhanga kwa hivyo hakuna mazungumzo kuhusu Ukraine yanayoweza kufanywa bila ya Ukraine kuwepo.