SiasaKyrgyzstan
Rais Vladimir Putin awasili nchini Kyrgyzstan
12 Oktoba 2023Matangazo
Kwenye ziara hiyo ya siku mbili, Putin anatarajkiwa kukutana na rais Sadry Zhaparov na kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola Huru, CIS, iliyoundwa baada ya kuanguka kwa uliokuwa Muungano wa Kisovieti.
Putin analenga kuimarisha ushawishi endelevu wa Urusi katika eneo la Asia ya Kati kama ilivyo kwa mataifa mengine yenye nguvu ya China, Marekani na Umoja wa Ulaya katika eneo hilo la kimakakati kati ya Ulaya na Asia.
Hii ni ziara ya kwanza ya Putin kwa mwaka huu tangu kutolewa kwa waranti huo wa ICC baada ya kuivamia Ukraine Februari 2022 na kumtuhumu kwa matukio kama ya utekaji na kuwaondosha watoto kwenye maeneo yanayokaliwa na Urusi nchini Ukraine.