1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Volodymyr Zelensky ataka Urusi kushinikizwa zaidi

19 Novemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameutolea wito Umoja wa Ulaya kuendelea kuishinikiza na kuibana Urusi kuelekea kile ilichokiita amani ya haki.

Ukraine Kiew 2024 | Präsident Selenskyj präsentiert Friedensplan im Parlament
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwasilisha Mpango wa Ushindi kwa Wabunge Kyiv, Ukraine, Oktoba 16, 2024 Ukraine.Picha: Ukraine Presidency via Bestimage/IMAGO

Zelensky ametowa mwito huo katika hotuba yake aliyoitowa kwa njia ya video,  mbele ya bunge la Ulaya kuhusu maadhimisho ya siku 1,000 tangu Urusi ilipoivamia nchi yake.''Kwa pamoja tumefanikisha mengi. Lakini hatupaswi kukhofia kuchukua hatua zaidi. Putin amewaleta wanajeshi 11,000 kutoka Korea Kaskazini na kuwapeleka katika maeneo ya mipaka ya Ukraine. Kikosi hiki huenda kikaongezeka hadi wanajeshi laki moja wakati baadhi ya viongozi wa Ulaya wakiwa bado wanatafakari kuhusu hilo,na wengine wakiwaza juu ya uchaguzi au mambo kama hayo, huku wakiitowa muhanga Ukraine,na Putin akilenga kushinda vita hivi. Hawezi kusitisha vita hivi kwa hiyari.''  Rais wa bunge la ulayaRobertaMetsola amesema Umoja huo utaendelea kusimama na Ukraine huku mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO Mark Rutte, ambaye amezungumza katika kikao cha mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya, akionya kwamba rais Vladmir Putin hapaswi kuachiwa kushinda nchini Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW