Zuma Berlin.
22 Aprili 2008
►◄
Rais wa chama kinachotawala nchini Afrika Kusini ANC Jacob Zuma amesema kucheleweshwa kutolewa matokeo ya uchaguzi nchini Zimbabwe ni jambo lisilokubalika na amewata viongozi wa Afrika wachukue hatua ili kusuluhisha katika mgogoro wa nchi hiyo.
Bwana Zuma amesema hayo leo mjini Berlin katika ziara yake fupi nchini Ujerumani.
Akizungumza katika mahojiano kiongozi huyo wa chama cha ANC amesema kuchelewesha kutoa matokeo ya uchaguzi hakuwasaidii watu wa Zimbabwe.
Watu wa Zimbabwe walipiga kura tareha 29 mwezi machi kulichagua bunge na rais, lakini matokeo ya uchaguzi huo bado hayajatangazwa hadi leo. Na hata zoezi la kuhesabu tena kura pia limecheleweshwa.Kutokana na hayo amewataka viongozi wa Afrika wachukue hatua ili wasuluhishe katika mgogoro wa Zimbabwe.
Amesema Afrika inapaswa kuchagua wajumbe watakaoenda Zimbabwe na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa pande zote ikiwa pamoja na wajumbe wa tume ya uchaguzi.
Katika ziara yake nchini Ujerumani kiongozi huyo wa chama cha ANC Jacob Zuma alikutana na bwana Kurt Beck mwenyekiti wa chama cha Social Demokratik kilichomo katika serikali ya mseto ya Ujerumani. Zuma anaefanya ziara ya nchi kadhaa za Ulaya anatarajiwa kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown kesho mjini London.
Pamaoja an mambo mengine sehemu kubwa ya aziara ya Zuma nchini Ujerumani imehusu mgogoro wa Zimbabwe