1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais wa Bangladesh alivunja bunge baada ya serikali kuanguka

6 Agosti 2024

Rais wa Bangladesh Mohammed Shahabuddin amelivunja bunge leo, na kusafisha njia ya kuandaliwa uchaguzi mpya wa kumpata mrithi wa waziri mkuu aliyetawala kwa muda mrefu Sheikh Hasina ambaye alijiuzulu.

Bangladesch | Raia Baadhi wakizungumza na DW
Baadhi ya Wabangladesh wakizungumza na DWPicha: Harun Rashid/DW

Hii ilifuatia wiki kadhaa za maandamano ya kupinga utawala wa Hasina ambayo yaligeuka kuwa ghasia. Rais Shahabuddin pia ameamuru kuachiliwa kwa kiongozi wa upinzani Khaleda Zia kutoka kifungo cha nyumbani. 

Zia, mpinzani wa muda mrefu wa waziri mkuu aliyeondolewa madarakani Sheikh Hasina, alihukumiwa kwa mashitaka ya ufisadi na serikali ya Hasina mwaka wa 2018. Baadhi ya nyadhifa kuu jeshini pia zimefanyiwa mabadiliko hii leo.

Soma pia:Waziri Mkuu wa zamani wa Bangladesh aachiliwa huru

Wanafunzi wanaoandamana wamesema hawataruhusu serikali yoyote itakayoungwa mkono na jeshi. Wakati huo huo, viongozi wa maandamano ya wanafunzi, kabla ya mkutano wao na mkuu wa majeshi leo, wamesema wanamtaka mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na muasisi wa sekta ya mikopo kwa wafanyabiashara wadogowadogo nchini humo, Muhammad Yunus, kuiongoza serikali hiyo. Yunus ana umri wa miaka 84. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW