1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Belarus Lukashenko asema Prigozhin amerejea Urusi

6 Julai 2023

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, ambaye mwezi uliopita alifanikisha makubaliano ya kumaliza uasi wa mamluki wa Wagner nchini Urusi, amesema kiongozi wa kundi hilo Yevgeny Prigozhin hayupo tena nchini Belarus.

Lukaschenko in Minsk
Picha: ALEXANDER NEMENOV/AFP/Getty Images

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, ambaye mwezi uliopita alifanikisha makubaliano ya kumaliza uasi wa mamluki wa Wagner nchini Urusi, amesema hii leo kuwa kiongozi wa kundi hilo Yevgeny Prigozhin hayupo tena nchini Belarus.

Lukashenko alisema wiki iliyopita kwamba Prigozhin alikuwa tayari amewasili nchini Belarus, lakini leo hii amesema Prigozhin amerejea nchini Urusi na sasa yupo St Petersburg.

Lukashenko amewaambia waandishi wa habari kuwa bado anashikilia pendekezo lake la kuwahifadhi wapiganaji wa Wagner nchini Belarus na ambalo lilizusha wasiwasi miongoni mwa mataifa ya NATO, na kwamba hana hofu kuwa mamluki wa Wagner siku moja wataivamia Belarus.