1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Benki ya Dunia asema kundi la G7 limeshindwa majukumu yake

Liongo, Aboubakary Jumaa7 Oktoba 2008

Rais wa Benki ya Dunia Robert Zoellick amesema kuwa mataifa saba tajiri duniani kwa sasa hayana tena nafasi na nafasi yake ichukuliwe na mataifa yanayokuja juu kiuchumi kama vile China, India na Brazil.

Rais wa Benki ya Dunia Robert ZoellickPicha: picture-alliance/dpa

Katika hotuba yake aliyoitoa mjini Washington kabla ya mkutano wa wakuu wa nchi hizo saba tajiri, mwishoni mwa wiki hii, rais huyo wa Benki ya Dunia amesema kuwa mzozo wa fedha unaoikumba dunia hivi sasa ni ishara ya kwamba wigo wa ushirikiano unatakiwa kupanuliwa zaidi.


Amesema kuwa kundi hilo la mataifa tajiri yaani G7 limeshindwa kazi na kwamba linahitajika kundi lingine bora zaidi, kwa wakati tofauti.                                                         


Kundi hilo la G7 linaundwa na nchi za Marekani, Uingereza, Canada,Ufaransa, Ujerumani, Italia na Japan.


Pia Rais huyo wa Benki ya Dunia Roberts Zoellick ametangaza kuwa ataunda tume itakayoongozwa na Rais wa zamani wa Mexico Ernesto Zedillo  kusaidia kuboresha muundo wa benki hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikidhibitiwa na Marekani.