1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Bulgaria aitisha uchaguzi wa bunge wa mapema

27 Agosti 2024

Rais wa Bulgraia ameitisha uchaguzi wa mapema wa bunge,mwezi Oktoba katika hatua nyingine ya juhudi za kujaribu kuuondowa mkwamo wa kisiasa na matatizo ya kiuchumi yanayolikabili taifa hilo.

Bulgaria | Uchaguzi wa bunge la Ulaya | Rais Rumen Radev
Rais wa Bulgaria Rumen Radev akipiga kura uchaguzi wa kitaifa na bunge la Ulaya Juni 2024Picha: Lin Hao/Xinhua/IMAGO

Rais wa Bulgraia ameitisha uchaguzi wa mapema wa bunge,mwezi Oktoba katika hatua nyingine ya juhudi za kujaribu kuuondowa mkwamo wa kisiasa na matatizo ya kiuchumi yanayolikabili taifa hilo mwanachama wa Jumuiya ya Nato na Umoja wa Ulaya.

Rais Rumen Rade ametangaza kwamba uchaguzi utafanyika Oktoba 27,ukiwa ni uchaguzi wa saba kuitishwa nchini humo katika kipindi cha miaka mitatu.

Soma: Bulgaria yanapiga kura uchaguzi wa tano katika miaka miwili

Pamoja na hatua hiyo, pia amemteuwa tena Dimitar Glavchev kuiongoza serikali ya mpito hadi utakapofanyika uchaguzi.Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwezi Juni na ulishindwa kutowa mshindi wa moja kwa moja. Bulgaria nchi ya wakaazi milioni 6.7 imekuwa ikiandamwa na misukosuko ya kisiasa  tangu mwaka 2020 baada ya kuzuka maandamano makubwa ya kuwapinga wanasiasa mafisadi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW