1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

Rais wa Burundi ateuliwa na chama chake kuwania Urais 2027

27 Aprili 2026

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ameteuliwa na chama chake cha CNDD-FDD kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao lakini tarehe rasmi haijatangazwa.

Bujumbura I Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye kutoka chama tawala cha CNDD-FDD akiwa mjini Bujumbura.Picha: Tchandrou Nitanga/AFP/Getty Images

Ndayishimiye mwenye umri wa miaka 57, ameiongoza Burundi tangu mwaka 2020, akichukua nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na kufuatia kifo cha mtangulizi wake Pierre Nkurunziza na atagombea kwa muhula mwingine wa miaka saba.

Rais Evariste Ndayishimiye  ambaye aliteuliwa Jumapili, amekishukuru chama chake kwa kumwamini na akaahidi kuendeleza sera na mipango kwa ajili ya maendeleo ya Burundi. Hata hivyo rais huyo anatazamiwa kuibuka mshindi huku upinzani wakisema kuwa uchaguzi huo hautakuwa wa huru na haki.

Epitace Nshimirimana, msemaji wa chama cha upinzani kilichopo uhamishoni cha MSD ameukosoa utawala wa Ndayishimiye akisema umeshindwa kutafutia jawabu suala la uhaba wa mafuta, fedha za kigeni na mahitaji ya msingi ya raia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW