Rais wa Chad amjibu kebehi rais Emmanuel Macron wa Ufaransa
7 Januari 2025Rais wa Chad Mahamat Idris Deby amemwambia rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwamba yuko katika enzi isiyomfaa, baada ya rais huyo wa Ufaransa kusema mataifa ya Afrika yalisahau kulishukuru jeshi la nchi hiyo lililopelekwa katika kanda ya Sahel kukabiliana na uasi wa makundi ya itikadi kali.
Rais Deby amemjibu Macro kupitia hotuba aliyoitowa ikulu na kuchapishwa kwenye ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Facebook, kwa kumwambia kwamba anaishi kwenye enzi nyingine asiyoijuwa.
Soma pia: Ivory Coast yawataka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka
Ufaransa hivi sasa inahangaika kutafuta namna ya kuendelea kubakisha uwepo wa jeshi lake barani Afrika baada ya kutimuliwa Mali, BurkinaFaso na Niger. Senegal na Ivory Coast pia zimeitaka nchi hiyo iondowe wanajeshi wake katika mataifa hayo.