1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Rais wa Chad Idriss Deby Itno afanya ziara nchini Hungary

8 Septemba 2024

Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby Itno aliwasili Hungary kwa ziara rasmi jana Jumamosi jioni, baada ya kuhudhuria kongamano la China na Afrika mjini Beijing mapema wiki hii. Haya ni kulingana na serikali ya Hungary.

Rais wa Chad  Idriss Deby Itno ahudhuria hafla ya kuapishwa kwake
Rais wa Chad Idriss Deby ItnoPicha: MOUTA/dpa/picture alliance

Msemaji wa serikali ya Hungary Zoltan Kovacs alichapisha picha za Rais Deby katika mtandao wa kijamii wa X akiwasili katika uwanja wa ndege wa Budapest.

Rais Derby kukutana na waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban

Wakati wa ziara hiyo rasmi, Rais Derby anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Hungary  Viktor Orban, ambaye ndiye mwenyeji wake. Ripoti za vyombo vya habari, zimeeleza kuwa viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadili makubaliano ya usalama.

Mahusiano kati ya Hungary na Chad yameimarika kwa kasi katika kipindi cha mwaka uliopita, huku Hungary ikifungua kituo cha msaada wa kibinadamu na maendeleo pamoja na ujumbe wa kidiplomasia katika mji mkuu wa N'Djamena.

Nchi hizo mbili pia zimetia saini mikataba ya ushirikiano kuhusu kilimo na elimu.