SiasaAsia
Rais wa China afanya mazungumzo na waziri mkuu wa Pakistan
7 Juni 2024Matangazo
Mzungumzo haya yanafanyika ikiwa ni siku kadhaa kabla ya Pakistan kutangaza bajeti yake ya kila mwaka na hatua ya kupeleka ombi jipya la kuomba mkopo katika shirika la fedha la kimataifa IMF.
Serikali ya waziri mkuu Sharif inatarajia kuomba takriban dola bilioni 6 chini ya mpango mpya wa IMF baada ya kuwasilisha bajeti yake ya mwaka ambayo kwa mujibu wa vyanzo huenda ikatangazwa Juni 10.
Soma pia:Kundi la Taliban lauteka mji wa 10 Afghanistan
Mkopo wa dola bilioni 27 ambazo Pakistan inadaiwa na China ndiyo suala kuu litakaibuka katika mazungumzo ya viongozi wa Islamabad na IMF.