Xi Jinping kuzungumza na viongozi wa kiarabu mjini Beijing
29 Mei 2024Miongoni mwa viongozi wa juu watakaoshiriki mkutano huo ni pamoja na rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi na rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan pamoja na viongozi wengine wa kikanda na wanadiplomasia.
Rais Xi Jinping anatarajiwa kutowa hotuba yake muhimu kesho Alhamisi atakapofunguwa mkutano huo unaolenga kupata msimamo wa pamoja kati ya China na nchi za Kiarabu.
Saudi Arabia yalaani mashambulizi ya Israel huko Rafah
Ajenda kuu ya mkutano huo ni vita kati ya kundi la wanamgambo la Hamas na Israel, ambapo rais huyo wa China ametowa mwito wa kufanyika mkutano wa kimataifa wa amani kuutatua mgogoro huo.
Kihistoria China imekuwa ikiunga mkono Palestina pamoja na mwelekeo wa kutaka suluhisho la kuundwa madola mawili,kumaliza mgogoro kati ya Israel na Palestina.