1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Rais wa China Xi Jinping afanya ziara nchini Morocco

22 Novemba 2024

Rais wa China Xi Jinping amefanya ziara fupi nchini Morroco baada ya kuhudhuria mkutano wa COP29 nchini Arzebeijan. Vyombo vya habari vya serikali za nchi hizo mbili, vimesema Xi, alifanya ziara hiyo jana Alhamisi.

Rais wa China Xi Jinping akihudhuria mkutano mjini Brasilia nchini Brazil mnamo Novemba 20,2024
Rais wa China Xi JinpingPicha: Adriano Machado/REUTERS

Katika ziara hiyo iliyolenga kuakisi uhusiano wa karibu, urafiki, ushirikiano, na mshikamano kati ya Morocco na China, Xi, alikutana na Mwanamfalme Moulay ElHassanhe. China imekuwa ikiwekeza zaidi katika miundombinu ya Morocco hasa reli katika miaka ya hivi karibuni.

Morocco inavutia wafanyabiashara wa China

Morocco ambayo iko karibu na Ulaya, na ambayo pia ina makubaliano ya biashara huria na Marekani na Umoja wa Ulaya pamoja na sekta ya magari, inavutia watengenezaji wa betri za magari ya umeme waChina.

Mnamo mwezi Juni, Kampuni ya kutengeneza betri ya Gotion High Tech ilichagua kujenga kiwanda chake cha kwanza kikubwa Afrika kitakachogharimu dola bilioni 1.3. za Kimarekani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW