1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Colombia ashinda tuzo ya Nobel

7 Oktoba 2016

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2016 kutokana na juhudi zake za kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya nusu karne.

Kolumbien Juan Manuel Santos Präsident Friedensnobelpreisträger 2016
Picha: picture-alliance/AP Photo/F. Vergara

"Rais Santos alianzisha majadiliano yaliopelekea kusainiwa kwa mkataba kati ya serikali ya Colombia na waasi wa kundi la FARC, na amekuwa akifanya juhudi za kupeleka mbele mchakato wa amani," ilisema kamati hiyo katika taarifa yake.

Tuzo hiyo inapaswa kuchukuliwa kama heshima kwa watu wa Colombia, kwa wale waliochangia mchakato wa amani, na kwa wawakilishi wa wathirika lukuki wa vita hivyo, ilisema kamati hiyo.

Vita vya wenyewe kwa wenye nchini Colombia - ambavyo ni mmoja ya vita vya muda mrefu zaidi katika zama hizi, vimegharimu maisha ya Wacolombia wasiopungua 220,000 na kuwakosesha makaazi watu wapatao milioni 6.

Tuzo hiyo yenye thamani ya dola 930,000, ilitolewa wakfu na mwanaviwanda wa Sweden na mgunduzi wa baruti Alfred Nobel. Mwaka uliyopita kundi la pande nne la majadiliano la Tunusia - ambalo ni muungano wa vyama vya wafanyakazi, mashirika ya watoa ajira, makundi ya haki za binaadamu na mawakili walishinda tuzo hiyo.

Mwandishi: Iddi Ssessanga

Mhariri: Saumu Yusuf

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW