Rais wa Colombia Petro apinga vitisho vya Trump
5 Januari 2026
Petro kupitia mtandao wa X amekanusha vikali madai hayo akisema jina lake halijaonekana kwenye rekodi za mahakama na amemtaka Trump aache kumkashifu.
Jana Jumapili, Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba atachukua hatua za kijeshi dhidi ya Colombia, baada ya kuishambulia Venezuela na kumuondoa Rais wake Nicolas Maduro kwa shutuma kama hizo za biashara ya dawa za kulevya.
"Kwa sasa tuna jirani mwenye hali mbaya. Sio jirani, lakini yuko karibu na jirani yetu. Inakera. Colombia ina hali mbaya pia, ikiongozwa na mtu asiyejitambua anayependa kutengeneza na kuuza dawa aina ya cocaine nchini Marekani. Lakini hataendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu. Ache niwaambie," alisema Trump.
Petro aidha amekosoa vikali hatua ya kijeshi ya utawala wa Trump nchini Venezuela na kuishutumu Washington kwa kumteka nyara Maduro "nje ya msingi wa kisheria."