1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Comoro aonekana baada ya kushambuliwa kwa kisu

19 Septemba 2024

Rais wa visiwa vya Comoro Azali Assoumani ameongoza hivi leo kikao cha baraza la mawaziri, ikiwa ni mara ya kwanza kuonekana hadharani tangu alipojeruhiwa katika shambulio la kisu wiki iliyopita.

Indien | G20 Gipfel in Neu-Delhi | Azali Assoumani
Rais Azali Assoumani akihudhuria mkutano kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya wakati wa Mkutano wa Viongozi wa G20 huko New Delhi Septemba 9, 2023Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Assoumani alionekana kwenye video akiwa na bandeji upande wa kushoto wa paji la uso wake huku akiwa na tabasamu kabla ya kupanda gari na kuwasili katika Ikulu ya rais.Kutoonekana kwa rais Assoumani kwenye sherehe za kidini za Maulidi ambalo ni tukio muhimu katika visiwa hivyo vidogo vya Afrika Mashariki vilivyopokwenye Bahari ya Hindi na vyenye watu 870,000 ambao wengi wao ni Waislamu, kulizua maswali mengi.Rais huyo mwenye umri wa miaka 65 alijeruhiwa na mwanajeshi ijumaa iliyopita wakati wa mazishi ya kiongozi wa kidini huko Salimani-Itsandra, viungani mwa mji mkuu Moroni.