SiasaVisiwa vya Comoros
Rais wa Comoro ampatia mwanae wa kiume wadhifa serikalini
2 Julai 2024Matangazo
Assoumani alitangaza bazara lake la mawaziri Jumatatu jioni ambamo pia alimteuwa Ibrahim Mohamed Abdou Razakou kuwa Waziri wa Fedha, Said Omra Houmadi kuwa Waziri wa Sheria na kumrejesha Yousoufa Mohamed Ali katika wadhifa wa Waziri wa Ulinzi.
Wachambuzi wa kisiasa, viongozi wa upinzani na vyombo vya habari vya nchini humo wanasema Assoumani alionekana kumuandaa El Fath mwenye umri wa miaka 40 kuchukua nafasi yake.
El Fath ni msomi aliyebobea kwenye masuala ya fedha na aliyefanya kazi kama mshauri mwandamizi wa kiuchumi wa rais huyo tangu 2019.