1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEl Salvador

Rais wa El-Salvador ajitangaza mshindi wa uchaguzi

5 Februari 2024

Rais wa taifa la El-Salvador Nayib Bukele amejitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika jana na kusema ameshinda kwa asilimia 85 ya kura, ingawa maafisa wa uchaguzi hawajatangaza matokeo rasmi.

El Salvador |Rais  Bukele
Rais wa taifa la El-Salvador Nayib BukelePicha: Alex Peña/Getty Images

Bukele mwenye umri wa miaka 42, amesema pia kuwa chama chake kinachoitwa "Mawazo Mapya" kimejishindia viti 58 kati 60 katika uchaguzi wa Bunge.

Rais huyo wa El-Salvador ndiye aliyetarajiwa kushinda hasa kutokana na kwamba wapiga kura, licha ya wasiwasi wao kuhusu mmomonyoko wa demokrasia walitaka kumpa muhula mwingine wa miaka mitano rais Bukele ambaye alipambana vikali na magenge ya wahalifu  na kuboresha usalama katika nchi hiyo ya Amerika ya Kati.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW