1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiGhana

Rais wa Ghana kuisubiri mahakama muswada dhidi ya mashoga

6 Machi 2024

Rais wa Ghana Nana Akufo Ado amesema serikali yake itasubiri uamuzi wa Mahakama ya Juu kabla ya kuchukua hatua yoyote kuhusu muswada wa sheria ambao utaongeza mbinyo dhidi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Rais wa Ghana Nana Akufo Ado
Rais wa Ghana Nana Akufo AdoPicha: Francis Kokoroko/REUTERS

Kiongozi huyo amesema anataka kuihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kuwa Ghana haitoipaka matope haiba yake ya kuwa taifa lenye rikodi ya kuheshimu haki za binadamu.

Muswada huo mpya unalenga kuongeza adhabu kwa jamii ya mashoga ikiwemo nyongeza ya kifungo gerezani kutoka miaka mitatu hadi 10 kwa wale wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Tangu ulipopitishwa umekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka makundi ya haki za kiraia ndani ya Ghana na kimataifa.

Vilevile kuna wasiwasi kuwa makopeshaji wakubwa wa nchi hiyo hususani Benki ya Dunia wanawezesha kusitisha misaada ya kifedha inayohitajika sana kuisaidia Ghana baada ya kipindi cha mdodoro wa uchumi.