Mkuu wa majeshi Guinea Bissau afutwa kazi
4 Desemba 2023Kiongozi huyo amesema hayo baada ya mkutano na vikosi vya usalama, ambapo alithibitisha kutokea kwa tishio hilo ambalo ni sehemu ya matukio yanayohujumu demokrasia katika eneo la Afrika Magharibi lililokumbwa na mapinduzi ya kijeshi.
Wiki iliyopita, kikosi cha wanajeshi kiliwatoa kizuizini bila ya kufuata utaratibu wa kisheria mawaziri wawili waliokuwa wamezuiliwa na polisi kwa tuhuma za rushwa, na kusababisha makabiliano ya risasi na vikosi maalum vya ulinzi wa rais.
Soma zaidi: Hali ya utulivu yarejeshwa nchini Guinea-Bissau
Wakati wa ziara katika kamandi ya wanajeshi wa ulinzi wa taifa mjini Bissau, Embalo alieleza kuwa mkuu wa majeshi Victor Tchongo ameachishwa kazi na kwamba "atalipa kwa gharama kubwa" kwa jaribio lake la mapinduzi.
Jaribio hilo la mapinduzi ni la pili katika eneo la Afrika Magharibi na Kati ndani ya muda wa wiki moja baada ya jaribio lengine lililoshindwa la wiki iliyopita nchini Sierra Leone.