1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya ziarani Ukraine

Angela Mdungu
4 Novemba 2023

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amewasili leo mjini Kyiv anakotarajiwa kulihutubia Bunge la Ukraine, kulingana na naibu wa bunge Yaroslav Zheleznyak.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: imago images/Armin Durgut

Ziara hiyo ya kushtukiza ya Von der Leyen inafanyika siku chache kabla ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Umoja wa Ulaya kuhusu hatua zilizofikiwa na Ukraine katika juhudi zake za kutaka kujiunga na Umoja huo.

Soma zaidi: Umoja wa Ulaya watofautina kuhusu msaada Ukraine

Tathmini hiyo iliyopangwa kuwasilishwa Jumatano inatarajiwa kueleza kwa kina jinsi Ukraine ilivyopiga hatua katika kutimiza vigezo kadhaa vikiwemo vya kiuchumi na kisheria ili kutoa nafasi kwa mazungumzo yatakayoanza mwezi Desemba. Ukraine iliyoomba kujiunga na Umoja wa Ulaya siku chache baada ya kuvamiwa na Urusi, inalipa kipaumbele suala la kujiunga na umoja huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW