1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran alitaka taifa kushikamana badala ya kuandamana

31 Desemba 2025

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amewataka raia wa taifa hilo, kuonyesha mshikamano badala ya kushiriki maandamano katika nyakati ngumu.

Iran Teheran 2025 | Masoud Pezeshkian
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, alitaka taifa kushikamana badala ya kuandamana katika nyakati alizoziita ngumu Picha: Iranian Presidency/ZUMA/picture alliance

Mwito wake umefuatia wimbi kubwa la maandamano ya umma yanayoshuhudiwa nchini humo tangu siku ya Jumapili kutokana na hali mbaya ya uchumi.

Rais Pezeshkian amesema taifa hilo linapitia mambo mengi ikiwemo shinikizo kutoa kwa maadui wa Jamhuri hiyo ya kiislamu, akisisitiza kuwa huu ni wakati wa raia kuungana kukabiliana na hali iliyopo na sio kuandamana.

Hata hivyo baadhi ya waandamanaji bado wanailaumu serikali kwa hali mbaya ya kiuchumi wakisema sera zake ndio sababu kuu ya mdororo wa uchumi katika taifa hilo lililo tajiri kwa mafuta na gesi.

Iran inahusisha maandamano ya siku nne nchini humo na njama za nchi za kigeni zinazolenga kuisukuma nchi hiyo katika machafuko na ukosefu wa utulivu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW