1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran awasili Urusi kusaini mkataba wa ushirikiano

17 Januari 2025

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amewasili nchini Urusi Ijumaa kwa mazungumzo na Rais Vladimir Putin pamoja na kusaini mkataba wa ushirikiano.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian -2024-Misri
Rais wa Iran Masoud PezeshkianPicha: president.ir

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amewasili nchini Urusi Ijuamaa kwa mazungumzo na Rais Vladimir Putin pamoja na kusaini mkataba wa  ushirikiano wa kimkakatikati ya nchi hizo mbili. Hii ni kulingana na Shirika la habari la seikali nchini humo TASS.

Mazungumzo yao yatajikita katika mahusiano ya mataifa yao na masuala ya kimataifa kabla ya kusaini makubaliano hayo.

Hii ni ziara ya kwanza ya Pezeshkian nchini Urusi tangu aliposhinda uchaguzi mwezi Julai mwaka uliopita baada ya kifo cha mtangulizi wake Ibrahim Raisi.

Urusi imekuwa ikitafuta ushirika na Iran na mataifa mengine hasimu wa Marekani kama Korea Kaskazini, tangu kuzuka kwa vita vyake nchini Ukraine na tayari imeingia makubaliano ya kimkakati na Pyongyang, mshirika wake wa karibu Belarus pamoja na China.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW