Herzog ataka dunia ipinge chuki dhidi ya Wayahudi
21 Desemba 2025
Rais wa Israel Issac Herzog ametowa mwito wa kufanyika kampeini duniani ya kupinga chuki dhidi ya Wayahudi.
Amesema hayo ikiwa ni wiki moja baada ya kutokea shambulio lililolenga tamasha la sikukuu ya wayahudi katika ufukwe wa Bondi nchini Australia, ambako watu 15 waliuwawa, wengi wakiwa wayahudi.
Viongozi wa dunia walaani kwa hasira shambulio la risasi Bondi Beach
Wito wa kiongozi huyo wa Israel, ameutowa wakati maelfu ya waombolezaji wakikusanyika katika ufukwe wa Bondi chini ya ulinzi mkali, hivi leo kukumbuka tukio hilo la mashambulizi yaliyofanywa na watu wawili waliokuwa na bunduki.
Viongozi mbali mbali wameshiriki kumbukumbu hizo akiwemo waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese. Herzog ameyaomba mataifa ya ulimwengu kuchukuwa hatua kali na madhubuti na kuonesha uongozi imara katika kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi.