Rais wa Italia ashinikizwa aitishe uchaguzi wa mapema
29 Januari 2008Matangazo
Washirika wa waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi, wamemshawishi rais wa nchi hiyo, Giorgio Napolitano, aitishe uchaguzi wa mapema.
Rais Napolitano amekuwa akifanya mashauriano ya dharura tangu waziri mkuu Romano Prodi alipojiuzulu wiki iliyopita.
Rais Napolitano huenda ateue serikali ya mpito iwapo makubaliano yatafikiwa kati ya vyama, hatua inayoungwa mkono na chama cha Romano Prodi.
Hata hivyo wazo hilo linapingwa na Silvio Berlusconi, ambaye wachambuzi wanasema huenda akanufaika iwapo kutafanyika uchaguzi wa mapema.
Berlusconi anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais Napolitano hii leo.