1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKazakhstan

Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev alivunja bunge

19 Januari 2023

Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev amelivunja bunge la nchi hiyo Alhamisi 19.01.2023 na kutangaza Machi 19 kuwa tarehe ya uchaguzi wa mapema.

St. Petersburg | Kasachstans Präsident Kassym-Jomart Tokajew
Picha: Gavriil Grigorov/Tass/dpa/picture alliance

Kulingana na taarifa iliyotoka katika afisi yake, Tokayev ameyavunja pia mabunge ya serikali za mitaa nchini humo. Katika ujumbe rais huyo amewaambia raia wa nchi hiyo kwamba anatarajia kuwa uchaguzi huo wa mapema utaleta "mwamko mpya" wa kuiendeleza nchi hiyo iliyo na utajiri wa mali asili, ambayo zamani ilikuwa katika muungano wa Sovieti.

Tokayev alichaguliwa mwezi Novemba baada ya kushinda asilimia 80 ya kura baada ya uchaguzi uliokosolewa kwa ukosefu wa ushindani. Aliahidi kuiunda Pakistan mpya yenye usawa ila changamoto za kiuchumi na mienendo ya kidikteta ndiyo mambo yanayoendelea kushuhudiwa katika utawala wake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW