1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Kenya afanya mabadiliko ya Baraza lake la Mawaziri

5 Oktoba 2023

Rais wa Kenya William Ruto amefanya hapo jana mabadiliko ya Baraza lake la mawaziri. Wizara mbalimbali zimeunganishwa na kubadilishwa jina.

William Ruto Kenia  Africa Climate Summit
Picha: Khalil Senosi/AP/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje Alfred Mutua amehamishwa katika wizara ya utalii na wanyamapori huku waziri wa biashara Moses Kuria akihamishwa kwenye wizara ya utumishi wa umma. Wizara ya mambo ya nje itakuwa chini ya mamlaka ya waziri mkuu Musalia Mudavadi.

Rais Ruto  amesema mabadiliko hayo yalikuwa muhimu ili kuboresha utendaji kazi kama ilivyoainishwa katika ilani ya utawala.

Ruto aliyeingia madarakani Agosti mwaka 2022, amekuwa akikabiliwa na msururu wa maandamano ya nchi nzima ambapo Wakenya wamekuwa wakilalamika kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha na ongezeko la ushuru.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW