1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Kenya amerejea sehemu kubwa ya mawaziri wa zamani

20 Julai 2024

Rais wa Kenya William Ruto amebadili kidogo baraza lake la mawaziri huku kukiwa na wito wa mabadiliko, ambapo sita kati ya mawaziri 11 waliokuwepo awali wanaendelea kuwepo serikalini.

Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya Wiliiam Ruto akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Nairobi Julai 04, 2024.Picha: TONY KARUMBA/AFP

Bado inaleta mashaka iwapo maamuzi haya yatapunguza hasira za vuguvugu la maandamano ya wiki kadhaa dhidi ya utawala wa Ruto na bado linamtaka ajiuzulu.

Maoni ya awali kwenye mitandao ya kijamii yalikuwa na mashaka kuhusu hatua hiyo itatekeleza serikali iliyoboreshwa iliyoahidiwa na Ruto katika msingi wa kuhusisha vyama vingi.

Zaidi ya hayo, upinzani katika nchi hiyo ya AfrikaMasharikiumegawanyika katika suala la ushiriki katika Baraza la Mawaziri la Ruto. Wanasiasa kadhaa wa upinzani wameitisha uchaguzi wa mapema.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW