Rais William Ruto awa Mwenyekiti mpya wa EAC
30 Novemba 2024Matangazo
Ruto ameidhinishwa katika mkutano wa 24 wa kilele wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo na atahudumu nafasi hiyo ya mzunguko kwa mwaka mmoja.
Katika hotuba yake ya kukabidhi nafasi hiyo Rais Salva Kirr amesema ulikuwa ni wakati mzuri kwake kuhudumu katika nafasi hiyo na amaanini majadiliano ya kuijenga Jumuiya imara yataendelea chini ya Ruto.
Mkutano huo pia umeidhinisha Kifaransa kuwa lugha rasmi, ikiifuatia lugha ya Kiswahili iliyoidhinishwa hivi karibuni.