1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Komoro alenga kumrithisha mwanawe madaraka

24 Januari 2025

Rais wa Komoro Azali Assoumani kwa mara ya kwanza amesema hadharani anakusudia kumrithisha madaraka mwanawe, Nour El Fath, wakati atakapoondoka ofisini mwaka 2029

Azali Assoumani
Rais wa Komoro Azali AssoumaniPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Kauli ya Rais Assoumani imethibitisha shutuma za wakosoaji ambazo zimekuwa zikienea kwa muda mrefu kwamba anamtayarisha mwanawe kuchukua nafasi yake.

Assoumani, ambaye kuchaguliwa kwake tena mwaka mmoja uliopita kulichafuliwa na madai ya ulaghai wa wapiga kura, yalimfanya El Fath kuwa msimamizi kuratibu mambo ya serikali na kumpa mamlaka makubwa juu ya baraza la mawaziri.

Akizungumzia wakati utakapofika wa yeye kuondoka madarakani,wakati wa hotuba kwa wafuasi wake katika kisiwa cha Moheli, Assoumani alisema atamuweka mwanawe kuchukua kama mkuu wa serikali na chama.

Abdallah Mohamed Daoudou, msemaji wa muungano wa upinzani nchini Komoro amesema kauli hio imeweka rasmi jambo ambalo tayari wanalijua, akihoji kwamba Azali anajidanganya mwenyewe, watu wa Komoro na wanasiasa hawatakubali kuwekewa utawala kwa nguvu ya nasaba au utawala wa kifalme katika kisiwa hicho.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW