Rais wa Komoro Mohamed Abdala Sambi ahutubia bunge la Tanzania
25 Agosti 2008Matangazo
Itakumbukwa kuwa serikali ya Tanzania ambayo ndiyo mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ilipeka kikosi chake kisiwani Nzouani ili kukikomboa baada ya Kanali Mohamed Bacar kukataa kuondoka madarakani.Kanali Mohamed Bacar alifanya uchaguzi kinyume na sheria mwezi Juni mwaka 2007.Umoja wa Afrika kwa upande wake ulieleza kuwa uchaguzi huo ulifanyika kinyume na sheria.Ili kupata picha halisi Thelma Mwadzaya amezungumza na Tausi Mbowe mwandishi wa habari aliyehudhuria kikao hicho cha Bunge mjini Dodoma.