Rais wa Kongo afungua njia ya kuachiwa mwandishi Bujakera
24 Februari 2024Matangazo
Hii ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi kusema kuwa mwandishi huyo ni mwathiriwa wa mfumo dhaifu wa utoaji haki.
Mwandishi huyo wa jarida la Jeune Afrique na shirika la habari la Reuters, amekuwa kizuizini tangu Septemba 8 kuhusiana na makala iliyohoji uhusika wa intelijensia ya kijeshi katika mauaji ya kiongozi mmoja wa upinzani.
Katika kikao cha waandishi habari Alhamisi usiku, Rais Tshisekedi alikosoa kile alichokiita kucheleweshwa makusudi kwa kesi hiyo na kusema ameamua kujiingiza katika suala hilo na kuahidi kuchukua hatua inayostahili kuchukuliwa.
Baada ya kuwasilisha ombi hilo, wakala wa Bujakera Jean-Marie Kabengela amesema kumekuwa na hatua iliyopigwa katika kesi hiyo.