Kiongozi wa Korea Kusini aliyetimuliwa aapa kupambana
2 Januari 2025Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa mamlakani Yoon Suk Yeol, ameapa kupambana hadi dakika ya mwisho sambamba na wafuasi wake waliopiga kambi katika makazi yake. Katika taarifa yake aliyoitoa jana Jumatano, Yoon amesema nchi hiyo ipo hatarini kutokana na nguvu za ndani na nje zinazotishia uhuru wake na shughuli za uasi dhidi ya serikali.
Soma: Rais wa Korea Kusini aondolewa madarakani na Bunge
Yoon ametoa matamshi hayo baada ya wachunguzi kusema jana kwamba watatoa waranti ya kumkamata kiongozi huyo baada ya kutangaza sheria ya kijeshi mwezi uliopita.
Wafuasi na wapinzani wa Yoon, ambaye aliondolewa madarakani na wabunge kutokana na jaribio lake la kutaka kupindua utawala wa kiraia, wamekita kambi nje ya makazi ambako amekuwa akizuiliwa kwa wiki kadhaa, wakizuia juhudi za kumhoji.