SiasaAsia
Rais wa Korea Kusini afikishwa mbele ya mahakama ya katiba
21 Januari 2025Matangazo
Rais Suk Yeol aliondolewa madarakani na bunge na kupokonywa majukumu yake mwezi Desemba baada ya kuitumbukiza nchi hiyo katika mkwamo wa kisiasa, kufuatia hatua yake ya kutangaza amri ya kijeshi.
Kadhalika kiongozi huyo amekuwa wa kwanza nchini humo, aliyeko madarakani kukamatwa akikabiliwa na uchunguzi wa kuhusika na uhalifu kwa misingi ya kufanya uasi.
Yoon Suk Yeol agoma tena kuhojiwa na timu ya wachunguzi
Ikiwa mahakama itapitisha uamuzi dhidi ya kiongozi huyo, atavuliwa urais na uchaguzi utalazimika kuitishwa ndani ya siku 60 zijazo.