1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLiberia

George Weah akubali kushindwa katika uchaguzi wa rais

18 Novemba 2023

Rais wa Liberia George Weah amekubali kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa rais nchini humo baada ya matokeo ya awali ya duru ya pili ya uchaguzi wiki

Rais wa Liberia George Weah akizungumza wakati wa mkutano wa COP27 huko  Sharm el-Sheikh, Egypt mnamo Novemba 8, 2022
Rais wa Liberia George WeahPicha: Peter Dejong/AP/picture alliance

Akilihutubia taifa kwa njia ya redio Ijumaa jioni, Weah alisema kuwa ingawa matokeo yaliyotolewa hadi wakati huo hayakuwa ya mwisho yanaashiria kuwa Bokai anaongoza kwa kiasi ambacho hawezi tena kumpiku. 

Maafisa wa uchaguzi wanasema wakati asilimia 99.58 ya kura zikiwa zimehesabiwa, Boakai alikuwa anaongoza kwa asilimia 50.89 dhidi ya asilimia 49.11% alizopata Weah. Matokeo hayo yalikuwa kinyume na matokeo ya uchaguzi wa miaka sita iliyopita, wakati Weah alipomshinda Boakai kwa urahisi katika duru ya pili.
 

Weah awataka wafuasi wake kukubali matokeo ya uchaguzi huo

Kiongozi huyo amewahimiza wafuasi wake kuiga mfano wake na kukubali matokeo ya uchaguzi huo akiongeza kuwa wakati wao utakuja tena mwaka 2029.

Hotuba hiyo ya Weah, imetolewa hata kabla ya matokeo rasmi kutangazwa nchini humo wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la wasiwasi kuhusu kuzorota kwa demokrasia katika mataifa ya Afrika Magharibi.
 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW