1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Liberia kupunguza mshahara wake kwa asilimia 40

9 Julai 2024

Rais wa Liberia Joseph Boakai ametangaza kuwa tayari kupunguza mshahara wake kwa asilimia 40 katika hatua ambayo inalenga kuweka mfano wa uongozi unaowajibika,katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Rais wa Liberia Joseph Boakai
Rais wa Liberia Joseph BoakaiPicha: Carielle Doe/REUTERS

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais,imesema hatua ya khiyari ya rais Boakai ya kupunguza mshahara wake inaakisi dhamira ya kuongoza kwa mifano ya kuimarisha uwajibikaji ndani ya serikali pamoja na kuonesha mshikamano na wananchi. 

Soma pia:Rais mpya wa Liberia Joseph Boakai aapishwa rasmi kuiongoza jamhuri kongwe zaidi barani Afrika

Boakai aliyeapishwa kuingia madarakani katikati ya mwezi Januari,  aliahidi kuimarisha hali za wananchi wa Liberia,kupambana na rushwa pamoja na kuheshimu utawala wa sheria.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW