Rais wa Marekani aahidi mzozo wa fedha utafumbuliwa na uchumi utaimarika
11 Oktoba 2008Washington:
Kwa mujibu wa rais George W. Bush wa Marekani,mataifa tajiri kiviwanda yatafanya kila liwezekanalo ili kumaliza mzozo wa fedha ulimwenguni.Kutokana na ushirikiano wa kimataifa,uchumi wa dunia utaimarika,baada ya mzozo huu wa sasa wa fedha,amesema hayo rais Bush baada ya mkutano pamoja na mawaziri wa fedha na wakuu wa benki wa mataifa sabaa tajiri kiviwanda G-7,katika ikulu ya White House mjini Washington.Jana mawaziri hao wa fedha na wakuu wa benki wa mataifa sabaa tajiri kiviwanda wameidhinisha mpango wa vifungu vitano uliolengwa kuikwamua hali ya mambo katika masoko ya fedha ulimwenguni.Mpango huo unazungumzia namna ya kuzihifadhi benki zisifilisike na kutengwa fedha za serikali ili kugharimia mikopo ikihitajika.Waziri wa fwedha wa serikali kiuu ya Ujerumani Peer Steinbrück amezungumzia juu ya "ishara bayana."Amedokeza serikali kuu ya Ujerumani itachangia katika mpango huo wa kuzinusuru benki zisifilisike.Kwa mujibu wa waziri wa fedha wa serikali kuu ya Ujerumani,mpango huo utaanza kufanya kazi jumatatu ijayo.