1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden azungumza na Mfalme wa Jordan kuhusu vita vya Gaza

27 Julai 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema pande zote zinafanya kazi kila siku ili kufanikisha makubaliano ya usitishwaji mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Rais wa Marekani Joe Biden akisalimiana na Mfalme wa Jordan Abdullah ibn Al Hussein
Rais wa Marekani Joe Biden akisalimiana na Mfalme wa Jordan Abdullah ibn Al HusseinPicha: Anna Moneymaker/Getty Images

Siku ya Ijumaa, rais wa Marekani Joe Biden amezungumza na Mfalme wa Jordan Abdullah kuhusu hatua zinazotakiwa kuchukuliwa ili kufikiwa kwa mpango huo wa usitishaji mapigano, kuachiliwa kwa mateka na kuongeza misaada ya kibinaadamu.

Soma pia: Mkutano wa dharura wazungumzia mzozo wa kiutu Gaza

Hadi sasa Hamas bado inawashilia mateka 111 ambao 39 kati yao wameripotiwa tayari kufariki. Mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel kufuatia shambulio la Oktoba 7 tayari yamesababisha vifo vya Wapalestina 39,175 huko Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW