1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Rais Biden amualika Waziri Mkuu wa Uingereza Sunak

14 Machi 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amemualika Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak katika Ikulu ya White House mwezi Juni mwaka huu

Italien Rishi Sunak und Joe Biden
Picha: Valeria Ferraro/SOPA/ZUMA Press/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden amemualika Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak katika Ikulu ya White House mwezi Juni mwaka huu.

Viongozi hao wawili watajadili mpango wa kuendelea kuwa na ushirikiano wa pamoja wa kiuchumi.

Mualiko huo umetolewa wakati viongozi hao walipokuwa San Diego, California, kuhudhuria uzinduzi wa mpango wa pamoja wa kununua nyambizi zinazotumia nguvu ya nishati ya nyuklia za Marekani.

Wakati wa mkutano wake na Rishi Sunak, Biden aliwaambia waandishi habari kwamba anapanga kutembelea Ireland na Ireland Kaskazini zinazojiandaa kuadhimisha miaka 25  ya makubaliano ya amani ya Ijumaa kuu Aprili 10.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW