1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Trump: Vita vya Iran vinaweza kudumu kwa wiki kadhaa

3 Machi 2026

Wakati vita vikiendelea Mashariki ya Kati, Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi kuwa taifa lake linao uwezo wa kuendelea na mashambulizi dhidi ya Iran kwa kipindi kirefu.

Tehran, Iran 2026 | Muonekano wa kituo cha polisi kilicholengwa katika mashambulizi ya Marekani na Israel mjini Tehran
Athari za mashambulizi ya Israel na Marekani mjini Tehran, IranPicha: Majid Asgaripour/WANA/REUTERS

Ameyasema hayo mjini Washington katika hotuba yake ya kwanza tangu vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iran vilipoanza.

Hayo yanajiri wakati ambapo Iran na washirika wake imeendelea kujibu mashambulizi dhidi ya Israel na katika nchi jirani za Ghuba.

Mashambulizi dhidi ya balozi za Marekani nchi za Ghuba

Mapema Jumanne imeushambulia ubalozi wa Marekani nchini Saudi Arabia kwa ndege mbili zisizo na rubani. Shambulio ambalo limefanywa baada ya kuulenga ubalozi mwingine wa Marekani nchini Kuwait Jumatatu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW