1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfilipino

Biden aihakikishia Ufilipino ushirika madhubuti wa kiulinzi

2 Mei 2023

Rais wa Marekani amemwambia mwenzake wa Ufilipino kwamba Marekani itaendelea kuwa mshirika wake madhubuti wa kiulinzi ikiwemo katika eneo la Kusini mwa bahari ya China.

USA Biden empfängt den philippinischen Präsidenten im Weißen Haus
Picha: Brendan Smialowski/Pool via AP/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden amemwambia mwenzake wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr  kwamba Marekani itaendelea kuwa mshirika wake madhubuti wa kiulinzi ikiwemo katika eneo la Kusini mwa bahari ya China ambako nchi hiyo ya Ufilipino inakabiliwa na shinikizo kutoka China. 

Rais Marcos Jr. ambaye ziara yake katika  Ikulu ya Marekani, ni ya kwanza kuwahi kufanywa na kiongozi wa juu katika kipindi cha miaka 10 wa Ufilipino amesisitiza juu ya umuhimu wa Marekani kama mshirika pekee wa nchi yake katika mkataba wa kiulinzi kwenye eneo hilo kutokana na kile alichosema hali tete ya siasa za kieneo zinazoshuhudiwa wakati huu.

Maafisa wa Marekani wamesema viongozi hao wawili wataingia kwenye makubaliano ya miongozo mipya katika ushirikiano imara zaidi wa kijeshi, pamoja na kuongeza ushirikiano wa kiuchumi.

Serikali mjini Washington inaitazama Ufilipino kama nchi muhimu  katika juhudi zozote za kuukabili uvamizi wa China wa Kisiwa cha Taiwan chenye mamlaka yake ya ndani ambacho China inadai kukimiliki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW