1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Mauritania ataka nguvu ya pamoja kuushinda ugaidi

23 Juni 2024

Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani ametoa wito kwa nchi za Afrika Magharibi kushirikiana katika kukabiliana na makundi ya wenye itikadi kali.

Mauretanien Mohamed Ould El-Ghazouani
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani akihutubia Mkutano Mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Septemba 20, 2023.Picha: AFP

Hayo kayasema katika mahojiano yake na AFP kabla ya uchaguzi wa rais wa Juni 29.Amenukuliwa akisema "Kanda lazima itengeneze nia ya pamoja ya kisiasa ili kuweza kupambana na ukosefu wa usalama." Aidha aliongeza kwa kusema hali ya usalama katika kanda hiyo sio nzuri hata kidogo na imeeendelea kuwa mbaya zaidi.

Mkuu huyo wa zamani wa jeshi na waziri wa ulinzi mwenye umri wa miaka 67 anatarajiwa kuhudumu kwa muhula wa pili kama mkuu wa nchi yenye watu milioni 4.5 ambayo iko kimkakati kati ya kaskazini na kusini mwa jangwa la Sahara.

Katika miaka ya hivi karibuni majeshi yalijitwalia mamlaka kwa nguvu katika nchi za Mali, Burkina Faso na Niger na hivyo kuzidisha hali ya sintofahamu katika eneo hilo. Taifa kubwa la jangwa la Rais Ghazouni lina pakana na Mali kwa mpaka wa zaidi ya kilomita 2,000.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW