Rais wa Mexico aahidi utulivu ufunguzi wa Kombe la Dunia
9 Juni 2026
Matangazo
Muungano wa walimu nchini humo umetishia kufanya maandamano makubwa kwenye mechi ya ufunguzi kati ya Mexico na Afrika Kusini itakayofanyika kwenye mji mkuu, Mexico City ikiwa serikali haitotimiza madai yao ya nyongeza za mishahara na pensheni.
Kwenye mkutano wake wa kila siku na waandishi habari, Bibi Sheinbaum amesema serikali yake itahakikisha sherehe za Kombe la Dunia zinafanyika katika mazingira ya amani na utulivu.
Wiki iliyopita, polisi iliwatawanya waandamanaji kwa mabomu ya machozi na risasi za mpira nje ya uwanja mkubwa wa Zocalo ambao umetengwa kwa mashabiki wasiokwenda uwanjani, kutizama mechi kupitia televisheni.