1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al Sissi na Guterres wajadili juhudi za kusitisha vita Gaza

21 Desemba 2023

Abdel Fattah Al- Sisi amejadili kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres juu ya juhudi kubwa zinazofanyika ili kuleta hatua ya kusimamisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza

Gaza Rauch steigt nach einem israelischen Angriff auf Rafah im südlichen Gazastreifen
Picha: Ismael Mohamad/UPI Photo/IMAGO

Wamezungumzia pia hatua ya kupelekwa misaada ya kutosha kwenye sehemu hiyo.

Hata hivyo katika tamko lake kundi la wanamgambo wa Hamas limesema hayatafanyika  mazungumzo juu ya kubadilishna mateka mpaka Israel itakapoacha mashambulizi.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laahirisha tena Azimio juu ya Gaza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa  kupitisha azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamasbaada ya kura ya azimio hilo kucheleweshwa kwa siku ya tatu mfululizo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW