1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Moldova

Rais wa Moldova akosoa uvamizi dhidi ya uhuru na demokrasia

21 Oktoba 2024

Rais wa Moldova Maia Sandu amekosoa kile alichokiita uvamizi dhidi ya uhuru na demokrasia wa nchi hiyo baada ya matokeo ya kura ya maoni kuonyesha kuwa raia wa nchi hiyo wanapinga kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Rais wa Moldova Maia Sandu
Rais wa Moldova Maia SanduPicha: Kommersant Photo Agency/SIA/picture alliance

Rais Sandu ameitoa kauli hiyo baada ya matokeo ya awali ya uchaguzi wa Jumapili kuonyesha kuwa asilimia 55 ya wananchi wa Moldova walichagua "hapana" katika kura ya maoni iliyotaka kuamua ikiwa Moldova inapaswa kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Kauli ya rais Sandu ambaye anaunga mkono taifa lake kujiunga na Umoja wa Ulaya na ambaye anaongoza katika uchaguzi wa rais imetolewa huku kukiwa na hofu ya kwamba Urusi ilingilia na kuvuruga matokeo ya uchaguzi huo.

Soma pia: Raia Moldova wapiga kura kumchagua rais, kuamua hatma ya kujiunga EU

Rais Maia Sandu amewaambia wafuasi wake katika mji mkuu Chisinau, kwamba Moldova imekabiliwa na shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa dhidi ya uhuru na demokrasia ya nchi hiyo na kuongeza kuwa makundi ya wahalifu yamejaribu kudhoofisha mchakato wa kidemokrasia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW