1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Msumbiji akutana na kiongozi mkuu wa upinzani

24 Machi 2025

Ofisi ya Rais wa Msumbiji imesema kuwa Rais Daniel Chapo amekutana na kiongozi mkuu wa upinzani Venancio Mondlane katika juhudi za kupunguza hali ya wasiwasi.

 Daniel Chapo na Venancio Mondlane
Daniel Chapo na Venancio MondlanePicha: ALFREDO ZUNIGA/AFP/Getty Images

Ofisi ya Rais wa Msumbiji imesema kuwa Rais Daniel Chapo amekutana na kiongozi mkuu wa upinzani Venancio Mondlane katika juhudi za kupunguza hali ya wasiwasi baada ya miezi kadhaa ya mapigano makali kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama.

Msumbiji ilifanya uchaguzi wake Oktoba mwaka uliopita na ambao waangalizi walisema uligubikwa na dosari na kupelekea maandamano yaliyogharimu maisha ya watu 360 kwa mujibu wa kikundi cha kiraia nchini humo.

Taarifa ya ikulu ya rais imesema Chapo na Mondlane wamekutana katika mji mkuu Maputo kujadili masuluhisho ya changamoto zinazokabili nchi hiyo.

Chapo aliingia madarakani mwezi Januari na mapema mwezi huu alitia saini mkataba wa baada ya uchaguzi na vyama vingine tisa kikiwemo chama cha zamani cha Mondlane cha Podemos.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW