1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ufisadi

Rais wa Msumbiji Nyusi kutoshtakiwa Uingereza

29 Februari 2024

Mahakama ya Rufaa ya London nchini Uingereza, imeamuru kuwa Rais wa Msumbuji Filipe Nyusi hawezi kushtakiwa nchini Uingereza kuhusiana na tuhuma za kupokea hongo.

Rais wa Msumbiji Philipe Nyusi
Rais wa Msumbiji Philipe NyusiPicha: Peter Dejong/AP/dpa/picture alliance

Mahakama ya Rufaa ya London nchini Uingereza, imeamuru kuwa Rais wa Msumbuji Filipe Nyusi hawezi kushtakiwa nchini Uingereza kuhusiana na tuhuma kuwa alikubali malipo kinyume cha sheria kama sehemu ya kesi ya Msumbiji kuhusu kashfa ya muongo mmoja iliyofahamika kama tuna bond, au hati za dhama za tuna.

Kampuni ya kimataifa ya kutengeneza meli ya Privinvest iliyoko Lebanon na Umoja wa Falme za Kiarabu ilitaka kumburuza Nyusi katika kesi ya dola bilioni 3.1 iliyofunguliwa na Msumbiji, ambayo inaituhumu kwa kutoa hongo kwa maafisa na wafanyakazi wa benki ya Credit Suisse.

Rais Nyusi, kushoto, anadaiwa kukubali malipo kinyumye cha sheriaPicha: Amós Fernando/DW

Soma pia:Rais wa zamani wa Msumbiji kutoa ushahidi kashfa ya rushwa

Privinvest ilitaka kumshitaki Nyusi kwa madai ya kukubali dola milioni 11 katika malipo ya kampeni kinyume cha sheria kutoka Privinvest, ambayo inasema malipo hayo yalikuwa halali.

Lakini Mahakama ya Rufaa imesema leo kuwa Nyusi hakufahamishwa ipasavyo kuhusu kesi hiyo.

Jaji Julian Flaux amesema katika uamuzi ulioandikwa kuwa Nyusi ana kinga ya kushtakiwa katika mahakama za Uingereza wakati akiwa rais wa Msumbuji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW